Salama Afunguka Makubwa Kuhusu Vanessa Mdee - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Salama Afunguka Makubwa Kuhusu Vanessa Mdee

Mtangazaji maarufu wa runinga na mchambuzi wa muziki Bongo, Salama Jabir, amefunguka kuwa Watanzania wategemee vitu vingi vikubwa kutoka kwa mwanamuziki wa kike Vanessa Mdee kwani bado ajaanza rasmi kujikita kwenye uimbaji ndio kwanza sasa hivi ni kama anafanya ‘Warm up’ vile (Kupasha mwili). Salama amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm, kuwa Vanessa ni msichana mwenye kipaji cha hali ya juu na atafika mbali zaidi.

Amedai kuna vitu na mipango ya Vanessa Mdee anayotaka kuianza ikiwemo staili ya uimbaji ambapo salama amesema anauhakika Vanessa akianza hiyo staili anayotaka kuizindua ataishangaza Tanzania. “Yani namuamini mno kwa sababu nae anajiamini, sasa hivi mbona bado ni kama anafanya Warm up vile, kuna vitu akivianza hivyo utaniambia, unajua Vanessa anaimba sana na atafika mbali” Alisema.


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.