Raymond: Kufanya Kazi na Chid Benz ni Bahati, Naona Nuru Kwenye Mziki Wangu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Raymond: Kufanya Kazi na Chid Benz ni Bahati, Naona Nuru Kwenye Mziki Wangu.

Msanii Raymond ameelezea furaha yake baada ya kufanya kazi na msanii wa hip hop Chid Benz, na kusema kuwa kwake ni bahati kubwa sana.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Raymond amesema yeye kufanya kazi na Chid Benz ni heshima kubwa, kwani msanii huyo ana uwezo mkubwa na yeye bado ni mchanga kwenye game.

"Nilifurahi kupata nafasi ya mimi kufanya ngoma na Chid Benz, kwa sababu ni brother ambaye alikuwa anafanya vizuri kitambo, ni msanii mzuri kwa hiyo mimi kufanya naye ngoma naona ni nafasi ambayo nimeipata inanionyesha kabisa kwamba muziki wangu unaenda kwenye nuru, kwa sababu mpaka kaka zako ambao walikutangulia wanakubali kufanya kazi na wewe, ina maana wanakubali kazi zako", alisema Raymond.

Raymond aliendelea kusema kuwa kazi hiyo ambayo ameifanya na Chid Benz ni wimbo aliotokea kuupenda sana, na kuahidi video mashabiki wake hivi karibuni.

"Ngoma ya chuma ni ngoma ambayo naipenda sana achilia mbali mtu ambaye nimefanya naye, namshukuru sana mungu na napata coments nyingi na soon video inakuja", alisema Raymond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.