Raymond Adondosha Machozi Baada ya Kupewa Gari na Diamond Platnumz. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Raymond Adondosha Machozi Baada ya Kupewa Gari na Diamond Platnumz.

Ilikuwa bonge la Surprise kwa msanii Raymond akiwa kwenye birthday yake, msanii huyu alipewa gari mpya na Bosi wake na kushindwa kujizuia mpaka kumwaga machozi.

Rayvanny aka Raymond amepewa gari mpya aina ya Rav4 na bosi wake wa WCB Wasafi Diamond Platnumz kama zawadi kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Raymond aliandika maneno haya kuhusu zawadi hii >> Kweli Nimeamini Mungu Hana upendeleo.nilikua mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani mi nne nilikua nikiangaika na muziki wangu nakushukuru sana sana kaka Lao @diamondplatnumz Umenifundisha vitu vingi saaaaaanaaa hadi leo naiona njia boss wangu @babutale Ni mwaka wa tano sasa toka Umenijua umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja.boss @sallam_sk Asante sana kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu nakuakikisha nafika sehemu nzuri @mkubwafellatmk wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha meeengi kwenye muziki @madeeali Sitoacha kukushukuru kaka lao wewe nikioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua saaaaanaaaa…ASANTENI SANA SANA SANA SANA MUNGU PEKEE NDIE ATAKAE WALIPA KWA WEMA HUU PESA PEKEE HAITOSHI #Godisgoodallthetime “

Sherehe ndogo ilifanyika nyumbani kwa Diamond, hii ndio gari alilopewa

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.