Q Chief: Jokate Alitosa Kutokea Kwenye Video Yangu Kwa Sababu Hii Hapa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Q Chief: Jokate Alitosa Kutokea Kwenye Video Yangu Kwa Sababu Hii Hapa.

Q Chief hamwezi Jokate Mwegelo. Ni kwasababu anadai imeshindikana kumtumia kwenye video yake kutokana na kile muimbaji huyo amedai mrembo huyo alitaka alipwe ‘six figures.’

Chief ambaye jina lake halisi Abubakar Katwila amedai kuwa amemtaja Jojo kwenye wimbo huo na kwamba ingemake sense kama angeonekana pia kwenye chupa lakini akawa ‘very expensive.’

Akiongea na E-News ya EATV Jumatatu hii, Chief alisema kuwa Jokate ni classmate wake hivyo alitarajia angemlegezea bei lakini Jojo only means business.

Pamoja na hivyo, muimbaji huyo anayejiita ‘Mungu wa Bongo Flava’ amedai kuwa anaheshimu uamuzi wa Jokate na ameongeza kuwa hawezi kuuondoa ukweli kuwa ni mtoto mkali.

Hivi karibuni Q alishoot video mpya na Justin Campos na kudai kuwa itawashangaza wengi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.