Pogba Asaini Mkataba wa Miaka 5 Manchester United. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Pogba Asaini Mkataba wa Miaka 5 Manchester United.

Paul Pogba amesema kuwa ni muda muafaka kurejea Old Trafford baada ya uhamisho wake wa Paundi 89 ulioweka rekodi ya dunia kwenda Manchester United.

Kiungo huyo mwenye miaka 23 anarejea tena klabuni hapo baada ya miaka minne alipoelekea Juventus kwa ada ya uhamisho wa paundi 1.5 mwaka 2012.
Pogba, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano ameongeza kuwa ''hii ni klabu sahihi kwangu kupata mafanikio ninayoyahitaji.''

Meneja wa Man U Jose Mourinho amesema Pogba atakuwa muhimili mkubwa wa klabu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho.

United itailipa Juventus ambao ni mabingwa wa Italia Euro 105 sambamba na Euro 5 ikiwa hii ikitegemea kiwango chake kitakavyokuwa.
Paul Pogba akiwa jijini Manchester

Pogba aliyeisaidia Ufaransa wenyeji wa michuano ya Euro 2016 kufika fainali ameshinda taji la Serie A katika miaka yote minne ndani ya klabu yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.