Pogba Amzawadia Drake Jezi Yake ya Juve - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Pogba Amzawadia Drake Jezi Yake ya Juve

Drake 1
STAA wa Soka wa Ufaransa anayetarrajiwa kujiunga na Klabu ya Manchester United ya uingeeza akitokea Juventus kwa uhamisho wa gharama kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani, akiwa ni miongoni mwa mashabiki wa ‘kufa mtu’ waliohudhuria show ya mwanamuziki Drake kwenye ukumbi wa Madison Square Garden, jijini New York, Marekani.
Drake 2
Pogba ambaye bado ni mchezaji wa Juventus yupo mapumzikoni nchini Marekani. Kiungo huyo mwenye miaka 23 ambaye hivi karibuni atakamilisha usajili wa paundi zaidi ya milioni 100 kwenda Man United alienda nyuma ya jukwaa na kumkabidhi Drake jezi ya Juve.
Pogba 2
Drake alikuwa akitumbuiza kwenye show ya ziara yake, Summer Sixteen. “Thanks to my bro @champagnepapi for this crazy performance last night .. #legend ah Oui hein #summersixteen #ovo,” aliandika Pogba kwenye picha akiwa na Drake aliyoiweka Instagram.
Kwenye picha nyingine inayomuonesha Drake akichukua selfie na Pogba, mchezaji huyo ameandika: Very nice meeting you bro @champagnepapi #holidays.”
Naye Drake ameshare picha kwenye Instagram akiwa na staa huyo na kuandika : When @paulpogba comes to see you that’s a 🌊
Mchezaji huyo anaonekana kufurahia mapumziko yake Marekani.
Pogba 3

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.