Picha: Ndege Mbili Zilizonunuliwa Na Serikali Hizi Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha: Ndege Mbili Zilizonunuliwa Na Serikali Hizi Hapa

Katika mwaka huu wa fedha 2016/17 serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo ndege hizo zitasaidia kuhuisha shirika hilo ambalo kwa sasa linamiliki ndege moja na nyingine ni ya kukodi zinazofanya safari katika baadhi ya mikoa nchini na kwenda Comoro.

Katika awamu ya kwanza ya ununuzi wa ndege hizo, serikali ilitenga 40% (TZS 39 bilioni) ya fedha zote na kununua ndege mbili Bombardier Q400 kutoka katika kampuni ya Bombardier Inc ya nchini Canada. Ndege hizo mbili zinatarajiwa kuwasili nchini mwezi Septemba mwaka huu.

Ndege mbili zilizonunuliwa katika awamu ya kwanza zinauwezo wa kubeba abiri 78 kila moja lakini zinatazonunuliwa katika awamu ya pili, kila moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiri 155.

Serikali imelenga kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa shirika hilo la ndege na kuhakikisha kuwa linajiendesha lenyewe. Ndege hizo zitakapowasili nchini zitaanza kufanya safari za ndani ya nchi kwanza.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za ndege zitakazonunuliwa na serikali katika awamu ya kwanza.Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.