Ommy Dimpoz na Alikiba Wana Colabo ? Zipo Hapa Picha Zao Wakiwa Location. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ommy Dimpoz na Alikiba Wana Colabo ? Zipo Hapa Picha Zao Wakiwa Location.

Ommy Dimpoz akiwa na models location Afrika Kusini.
Ommy Dimpoz na Alikiba wanaweza kuwa wanajiandaa kuja na wimbo wa pamoja siku si nyingi. Na In fact, picha zao kwenye Instagram zinaonesha tayari wameshoot video hiyo.

Alikiba ndiye aliyeanza kupost picha hiyo chini kwenye Instagram na kuandika kwenye caption #Kajiandae.
Baadaye Ommy alikuja kupost picha tatu ikiwemo hiyo juu ya kwanza na kuiweka hashtag ya #Kajiandae hali inayoonesha kuwa ni wimbo wa pamoja wa wawili hao. Kuna kila dalili kuwa video hiyo imefanyika Afrika Kusini.
Hii haitakuwa mara ya kwanza wawili hao wanafanya wimbo pamoja. Ommy alimshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake Nai Nai uliomtambulisha kwenye muziki wa Tanzania.

Hii itakuwa ngoma inayokuja huku mashabiki wa Alikiba wakiwa na kiu na shauku ya ngoma mpya kutoka kwake kwani baadhi yao wanadai kuwa anachelewa sana kutoa ngoma mpya. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.