Obama: Kama Trump Atashinda Urais, Nitaihama Marekani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Obama: Kama Trump Atashinda Urais, Nitaihama Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa iwapo mgombea urais wa Chama cha Republican, Donald Trump atashinda katika uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo yeye ataondoka Marekani.

Barack Obama Rais wa Marekani ameliambia Gazeti la World News Politics kwamba, kama Trump atashinda uchaguzo ujao wa rais, yeye na familia yake wataondoka Marekani bila ya mapema.
Mgombea urais wa Chama cha Republican, Donald Trump

Obama amesema kuwa amejadiliana na mke na watoto wake kuhusu suala hilo la kukubaliana kwenda nje ya Marekani iwapo Trump atashinda kiti cha rais wa nchi hiyo.

Inasemekana kwamba, iwapo ataondoka Marekani, Rais Obama anakusudia kuishi nchini Canada na kwamba tayari maudhui ya kuhama kwa Obama imejadiliwa na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau.

Matamshi na misimamo ya kushangaza ya mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump imekabiliwa na upinzani mkali ndani na nje ya Marekani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.