Nuh Mziwanda Adaiwa Kupigwa Ndoa ya Mkeka. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Mziwanda Adaiwa Kupigwa Ndoa ya Mkeka.

Staa wa Ngoma ya Jike Shupa, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupigwa ndoa ya mkeka na wazazi wa mpenzi wake ajulikanaye kwa jina moja la Nawali, kufuatia wazazi wa binti huyo kuchoshwa na uchumba hewa wa mtoto wao ambapo msanii huyo alijimilikisha bila utaratibu.

Chanzo makini kililiambia Wikienda kuwa, ndoa hiyo ilifungwa kwa siri usiku, mwishoni mwa wiki iliyopita huku mwanamuziki huyo akiwa hajaridhia kufanya tukio hilo.

Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Wikienda lilimtafuta Nuh na kumuuliza ishu hiyo ambapo aliruka futi mia moja, akidai muda muafaka ukifika atafanya hivyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.