Msanii Mirror Apata Ajali - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Mirror Apata Ajali

MSANII wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Endless Fame inayomilikiwa na malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Mirror amepata ajali maeneo ya Ununio jijini Dar hivi punde.

Inasemekana, Mirror alikuwa akielekea nyumbani kwa bosi wake, Wema ‘Madam’ na baada ya kufika maeneo hayo alipata ajali mbaya iliyosababisha gari alilokuwa nalo, (gari ndogo aina ya Toyota lenye namba T 169 DDK) kutumbukia katika mtaro.

Inasemekana Mirror alikuwa peke yake ambapo baada ya ajali alipata maumivu makali maeneo ya miguuuni na hapohapo alipopigiwa simu Wema hakupatikana hewani na alipopigiwa Kadinda iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo wasamaria wema wamemchukuwa na kumuwaisha hospitali kwa matibabu zaidi.

Kwa habari zaidi ya kitakachoendelea tutazidi kuwajuza, endelea kufuatilia mtandao huu.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.