Linah: Sina Uhusiano wa Kimapenzi na Billnass - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Linah: Sina Uhusiano wa Kimapenzi na Billnass

Msanii wa muziki, Linah Sanga amekanusha tetesi ambazo zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na rapper Billnas.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Billnas ni mshkaji wake.

“Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na BillNas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana,” alisema Linah “Saizi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu,”

Aliongeza, “Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’ na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo,”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.