Juma Nature: Haitatokea Nikalia Kwa Sababu ya Mapenzi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Juma Nature: Haitatokea Nikalia Kwa Sababu ya Mapenzi.

Star wa muziki na Mkongwe wa Bongo Flava, Juma ‘Nature’ Kiroboto, amefunguka na kudai kuwa kwa sasa haitatokea akalia kwa sababu ya Mapenzi.

Akiongea kupitia kipindi cha Hatua Tatu jana asubuhi, Nature amedai aliwahi kulia kipindi ambacho anachipukia katika mahusiano ila kwa sasa hakuna Mwanamke atakaeweza kumliza. “Nimewahi kulia lakini kipindi nipo mdogo, zamani sana si unajua nilikuwa nachipukia nini, ila kwa sasa nimeshakuwa hakuna Mwanamke atakaeniliza kwenye mapenzi hata siku moja” Amesema.

Katika hatua nyingine mkali huyo, amesema kwa sasa hawezi kufanya kolabo na Naseeb ‘Diamond’ Abdul, mpaka pale watakapofanya mpambano wao kwenye show ya Pamoja.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.