Je, Unajua Kama Unawezaje Kutumia Fikra Zako Kupata Unachokitaka ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Je, Unajua Kama Unawezaje Kutumia Fikra Zako Kupata Unachokitaka ?

Fikra za binadamu zina uwezo mkubwa sana katika kufanya maendeleo, fikra zinaendesha maisha ya mtu binafsi, lakini je huwa ni fikra gani zinakutawala? Inasemekana kuwa kila unachokitaka kinaweza kutokea kama tu utaruhusu fikra zako ziwaze kitu unachotaka.

Tumia akili yako kuwaza vitu chanya (Positive), upo wakati binadamu anawaza vitu visivyo na mafanikio, vitu vya kuhuzunisha au vitu vya kutia hasira, hii inakusababishia mawazo na maumivu (stress) kwa sababu ya kuwaza tu ugonjwa unaweza kuumwa, kuwaza kama chakula ni kibaya au kimechacha, unaweza kuumwa tumbo hata kuhara,

Hiyo ni mifano tu midogo ambayo watu wengi hukutana nayo bila kujua kama wao ndio wanasababisha matatizo hayo, mfano mwingine mzuri ni kuangalia Filamu za kutisha na ukajikuta unaota wadudu au majini wa filamu ile wanakufwata hii ni kwasababu fikra za uoga zimekujaa na kuanza kuwaza kile ulichokiona.

Wanasema, kuwa makini na unachoruhusu kiingie akilini mwako hii si kwa filamu tu unazoangalia, bali hata kwa nyimbo na watu unaowasikiliza kila siku, aina ya stori unapenda kusikiliza na vitu kama hivyo, kila unachokiingiza katika akili au fikra zako kina mchango mkubwa wa kukufanya uwe wewe ulivyo sasa.

Kama unataka mafanikio anza kuyakumbatia mambo yanayoendana na mafanikio soma na angalia vitu vitakavyokusaidia kwa namna moja au nyingine kutimiza ndoto zako, fikiria ndoto na malengo yako mara kwa mara ruhusu fikra yako kujenga ndoto yako kwanza, hata anae nunua gari huwa na picha akili mwake ya aina ya gari anayoitaka. Weka picha ya kitu unachokitaka akilini mwako kwanza.

Ridhika kwa kile ulichonacho, wakati unawaza juu ya vingine vingi unavyohitaji,usijiwekee mashaka, usiwaze vikwazo usiwaze kufeli waza kufanikiwa na utaona maajabu, Amini Fikra zako zina Nguvu ya ajabu katika maisha yako ya kila siku. Fikra zako zitakupatia gari, nyumba,au maisha unayoyafikiria.

-Rabiadamary (mmasaimfupi)

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.