Harmonize: Kidogo Nachopata Kinatosha Kumhudumia Baby Wangu Wolper. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize: Kidogo Nachopata Kinatosha Kumhudumia Baby Wangu Wolper.

Msanii wa muziki wa label ya WCB, Harmonize amefunguka kwa kusema kuwa kidogo anachokipata katika muziki wake lazima ahakikishe anakula na baby wake ili kulinda status yake.

Muimbaji huyo ambaye anatoka kimapenzi na staa wa filamu, Jacqueline Wolper, amesema gharaza za kumtumza mrembo huyo hazimsumbui kama watu wanavyofikiria.

“Suala la kinywaji vyumbani kwake ana kaunta, so akijisikia kunywa anakunywa nyumbani, mimi nirudi studio namkuta anakunywa, na hajawai kuniambia sijui anatoka na mashoga zake,” Harmonize alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Aliongeza, “Mwanamke yupo kwa ajili ya mwanaume anayempenda,so kidogo nachokipata lazima nihakikishe namlinda baby wangu, nalinda status yake. Kwa sababu usipo mhudumia mwanamke wako, atamhudumia nani? atamhudumia mtu mwingine, so kidogo nachokipata nakitunza kuhakikisha baby wangu anapendeza vizuri na anakula anachokitaka. Lakini sidhani kama kuna mwanaume mjinga ambaye anaweza kutelekeza familia yake kwa ajili ya mwanamke, kwa sababu sidhani bila Mama yangu kunizaa na kunituza ningemjua mwanamke, so kwanza Mama yangu halafu inakuja familia yangu, na kwa sababu mwanamke wangu ni sehemu ya familia yangu,”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.