Fid Q: Maisha ya Nyuma Ndio Yaliyonipa Idea Ya Ngoma 'Roho' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Fid Q: Maisha ya Nyuma Ndio Yaliyonipa Idea Ya Ngoma 'Roho'

Rapa na mkali kutoka jijini Mwanza ambaye anafanya muziki wa Hip Hop hapa nchini amefunguka kuhusiana na mashairi aliyoyaandika kwenye wimbo wa Roho kwamba kile kilichomo ndani ni mahusiano aliyokuwa akiishi na mpenzi wake wa kwanza na hivyo ndio sababu ya kuandika mistari yenye hisia zote zile.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha Redio cha East Africa, Farid amesema wakati anaingia studio kuandaa wimbo huo alikuwa akitaka kuandika ngoma ambayo itazungumzia mapenzi kwa ujumla lakini akiwa studio akakumbukia maisha ya nyuma na hivyo kujikuta tu anashusha mistari ya wimbo wake.


“Kiukweli nilitaka kuandika kuhusu wimbo wa mapenzi lakini wazo halikuwa limekaa vizuri bado, kuna kipindi nikataka nielezee kuhusu kupendwa lakini nikaona zimeshaandikwa sana nyimbo hizo, nikiwa nimetulia nikakumbuka mbali sana kuhusu haya haya mapenzi nikaumiza kichwa na kushusha mistari” alieleza Fid Q

Akifafanua juu ya kuamua kumchagua Christian Bella katika ngoma hiyo, Fid Q amesema kuwa yeye ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa muziki wa Bella na hata alipomuita kufanya nae kazi akagundua kweli mtu aliyemuweka ni sahihi katika kazi hii.

“Mimi namkubali sana Bella na ni moja kati ya mashabiki wakubwa sana wa muziki wake, na lilipokuja swala la kumchagua nani akae katika nyimbo hii Bella alikuwa namba moja na halikuwa na mpinzani swala hilo, nilichofanya nikamuachia yeye mwenyewe atie wino wake mwenyewe katika kuhakikisha anaweka melody zake sawa na kitu kikawa SUMU,” aliongeza Fid Q

Fid Q ambaye kwa kipindi cha nyuma alifanya vizuri na nyimbo yake ya`Walk It Of` aliyomshirikisha Producer Taz ameachia ngoma mbili, moja ikipewa jina la Roho akiwa amemshirikisha Christian Bella na nyingine akiipa jina la Sumu ambayo bado hajaifanyia video.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.