Dj Khaled na Black Chyna Wamemfanyia Wema Sepetu Kitu Hiki Hapa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dj Khaled na Black Chyna Wamemfanyia Wema Sepetu Kitu Hiki Hapa.

Ukizungumzia page ambazo zinafuatwa zaidi katika mtandao wa Snapchat huwezi kuacha kuitaja ile ya Dj mkali sana nchini Marekani na Dunia nzima kwa ujumla Dj Khaled.

Ni page ambayo watumiaji wengi wa mtandao huo wana wanaifuata kutokana Dj huyo kuyaonyesha mambo mengi ambayo anayafanya katika maisha yake ya kila siku katika page yake hiyo.

Kibongo bongo ukizungumzia watu ambao pia wanakichafua kwa kufuatwa na watu wengi katika mtandao huo pia huwezi kuacha kumtaja mwanadada Wema Sepetu, kwasababu ni mtu ambae ana fanbase ya kutosha kwa ukanda huu na pia mwenye ushawishi mkubwa na hivyo kuwafanya watu wengi kumfuata (Kumfollow) katika mitandao yake ya kijamii.

Sasa leo mwanadada Wema Sepetu ametusanua kuwa mastaa wakubwa Duniani Dj Khaled na Black Chyna wame mfollow katika account yake ya Snapchat.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.