Diamond Platinumz: Mafanikio Hayapo Kwenye Muziki Tu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Platinumz: Mafanikio Hayapo Kwenye Muziki Tu

Msanii wa muziki wa Bongo Flava Diamond Platinumz amesema mafanikio hayapo katika muziki tuu bali kila mtu anatakiwa kuangalia mahali ambapo pana upungufu na kujitahidi kufanyia kazi hilo eneo ndipo ataweza kutoka kimaisha.

Akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX Diamond amesema wakati anaingia kwenye tasnia ya muziki kuna watu ambao walikuwa wanafanya vizuri kwenye Bongo Movies kama Steven Kanumba, watangazaji, wanamichezo mfano Mbwana Samatta na wengine wanafanya vizuri kwa kuangalia upungufu uliopo sehemu na kuufanyia kazi kwa bidii hivyo vijana wasikimbilie muziki tu wakiamini ndiyo unaweza kuwatoa kimaisha.

‘’Ukiachilia mbali kazi ya muziki mimi pia nina vikorokoro kibao ambavyo vinaniwezesha kuweza kupata kipato ch kil siku hivyo si kwamba muziki ni kila kitu lazima kujishuhulisha na Mungu anasaidia kuweza kusonga mbele’’ Amesema Diamond.

Aidha msanii huyo amesema pamoja na kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania anajitahidi sana kuhakikisha kila anachokifanya hakiharibu mila na desturi za watanzania.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.