Diamond Kufanya Ziara ya Afrika Akiwa na Bendi Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Kufanya Ziara ya Afrika Akiwa na Bendi Yake

Hatimaye Diamond ameamua kusikiliza kilio cha wengi kwa si tu kuanzisha bendi yake, bali pia kujiandaa kwa ziara ya Afrika.

Muimbaji huyo amepost video kadhaa zinazomuonesha akiwa mazoezini na bendi hiyo na kueleza kuwa ni maandalizi ya ziara yake ya Afrika.

Miongoni mwa watu wanaonekana kwenye bendi hiyo ni producer, Tudd Thomas.

Ziara hiyo inakuja katika kipindi ambacho staa huyo anajiandaa kuachia album yake ya kwanza ya kimataifa.

Pia ndio itakuwa ziara yake ya kwanza ya uhakika kuzunguka bara hilo. Bado hajesema itaanza lini na wapi.

Kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakimshauri aanze kutumbuiza na live band hasa kwenye show zake za kimataifa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.