Diamond Adai Alikuwa Muuza Mitumba ‘Nilikuwa Najipitisha Kwa Bob Junior na AliKiba ili Wanunue’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Adai Alikuwa Muuza Mitumba ‘Nilikuwa Najipitisha Kwa Bob Junior na AliKiba ili Wanunue’

Mkali wa wimbo ‘Kidogo’ Diamond Platnumz amefunguka na kueleza jinsi alivyoweza kupambana na biashara ndogo ndogo ya kuuza mitumba wakati anatafuta njia yakutoboa.

Muimbaji huyo amesema Bob Junior na Ali Kiba ni moja kati watu ambao alikuwa anapenda kuwaonyesha mara kwa mara biashara yake.

“Unajua mimi nilikuwa nakutana sana na Bob Junior pale kwao ilipokuwa ‘studio’ kwa sababu nilikuwa nauza nguo maeneo yao pale, sasa yeye alikuaga anapita na akina Ali pale nawaonyesha onyesha nguo najua hawa ma brazameni ili mimi nipige hela,” alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.

Kwa sasa Diamond ni mmoja kati ya msanii mwenye mafanikio makubwa katika muzuki nchini Tanzania.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.