Darassa: Video ya ‘Too Much’ Ilinitoa Jasho Sana. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Darassa: Video ya ‘Too Much’ Ilinitoa Jasho Sana.

Rapper ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake, ‘Too Much’ Darassa, amesema video ya wimbo huo ilimtoa jasho.

Akiongea na kipindi cha Funiko Base cha Radio 5, Darassa alisema imemchukua muda mwingi na pesa nyingi kuikamilisha video hiyo kwakuwa alitaka kufanya kitu kikubwa.

“Too Much kwangu ni video kubwa na imetucost,imetuchukua muda,imetuumiza hapa ninavyoongea hakuna tulichobakiwa nacho zaidi ya nguvu na akili tu,” alisema.

“Tulichokuwa tunataka ni kuhakikisha tunatengeneza video nzuri nyumbani hata tukifanikiwa kimataifa watu wajue jamaa ameendelea tu ila alianzia nyumbani ndio tunachopambania,watu wa nje wahitaji kufanya kazi na sisi.”

Video ya wimbo huo iliongozwa na Hanscana.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.