Aunt Ezekiel Akiona cha Moto Dodoma ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Aunt Ezekiel Akiona cha Moto Dodoma !

STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel hivi karibuni alikiona cha moto kwenye mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma baada ya kutolewa ukumbini kwa nguvu.

Kwa mujibu wa chanzo, wasanii wote walitakiwa kuwa na vitambulisho maalum vya kuingilia ukumbini ambapo Aunt hakuwa nacho badala yake akapewa cha watu wa usalama wa Taifa.

Baada ya kuingia nacho alishtukiwa na kutolewa nje kwa nguvu kitu kilichomlazimu kurejea hotelini.

Gazeti hili lilimtafuta Aunt aliyekiri kutoingia ukumbini kwa sababu shosti wake Kajala alikuwa anaumwa na si vinginevyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.