Alikiba Msanii wa Kwanza TZ Kutokea Kwenye Jarida la The Source la Marekani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Msanii wa Kwanza TZ Kutokea Kwenye Jarida la The Source la Marekani.

Alikiba atakuwa msanii wa kwanza kutokea kwenye jarida maarufu la The Source la nchini Marekani.
The Source ni jarida maarufu kwa hip hop na limekuwa na heshima kubwa kwa muda mrefu. Kiba atakuwa mmoja wa wasanii wachache sana wa Afrika kuwahi kuandikwa kwenye jarida hilo.

Ameshare habari hiyo njema kwenye mtandao wa Instagram.

“The 1st Bongo Flava artist in history to be featured in the THE SOURCE MAGAZINE! I’m proud to place BongoFlava on cover feature of the number #1 MusicMag on the Planet,” aliandika msanii huyo wa Sony Music.

Hata hivyo hajasema makala yake itatokea kwenye toleo la mwezi gani.
The Source hutoka kila mwezi na kuandika zaidi habari za hip hop, utamaduni na siasa na lilianzishwa mwaka 1988. Ndio jarida la rap lililodumu kwa miaka mingi zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.