Afande Sele: Adhabu ya Babu Tale Kulipa Shilingi Milioni 250 Ni Ndogo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Afande Sele: Adhabu ya Babu Tale Kulipa Shilingi Milioni 250 Ni Ndogo.

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele amefunguka kwa kusema kuwa adhabu ya shilingi milioni 250 aliyopewa Babu Tale ni ndogo.

Meneja huyo wa Tip Top Connection, anatakiwa alipe kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo.

Afande amedai kiasi hicho alichoamriwa kulipa ni kidogo kutokana meneja huyo wa Diamond kuushika muziki wa bongofleva.

“Inawezekana faini ya shilingi million 250 alizoamriwa Babu Tale na Mahakama Kuu ya Tanzania amlipe yule Sheikh mwenye madai dhidi yake Tale na nduguye ni ndogo sana kwao ukizingatia yeye Tale ndio meneja wa wamiliki wa bongofleva kwa sasa. Lakini ukweli ni kwamba pesa yeyote inayotoka bila kuingia wala kutarajia inauma sana,” aliandika Afande kupitia facebook.

Aliongeza, “Pole sana wakunyumba Babu Tale naamini haya ni mapito katika maisha na yatakwisha ingawa upande wa pili ni mafunzo kwetu wengine tunaojiona na kujiita wajanja wa mjini kuwa sheria ni msumeno na mahakama ni kama nyoka usimdharau kwa udogo wake wa umbo au umri, wote wanasumu na sumu humuua yeyote!,”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.