Wema Sepetu Amtesa Idris, Hii Ndio Sababu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Amtesa Idris, Hii Ndio Sababu.

Mpenzi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, Idris Sultan alijikuta katika wakati mgumu wa kuhakikisha analiweka vizuri gauni refu la mrembo huyo kila alipokuwa anakwenda.

Ishu hiyo ilitokea hivi karibuni katika Ukumbi wa King Solomon uliopo maeneo ya Namanga jijini Dar kulipokuwa na pati maalum iliyofahamika kwa jina la Black Tie ambayo iliandaliwa na Madam kuadhimisha miaka kumi ya mkali wa dansi Bongo, Christian Bella.
Awali, kabla ya Madam kumhenyesha Idris, kulitanguliwa na shoo ya utangulizi ya Bella ndipo wapendanao hao walipopanda jukwaani kwa madoido kwa ajili ya utambulisho wa wao kuwa ma-MC wa shughuli hiyo.

Wakati wanapanda ngazi za jukwaa hilo, licha ya Madam kuwa na wapambe wake (warembo) waliokuwa wakishikilia gauni hilo, bado Idris aliyekuwa amemshika mkono Madam alilazimika kulishikilia gauni hilo kumfanya mpenzi wake huyo aweze kutembea vizuri.
“Mh! Lile gauni la Madam mwenzangu linamtesa kweli leo Idris maana tangu wanapanda ngazi hadi alipofika jukwaani bado anahangaika nalo ili kumfanya baby wake awe ‘comfortable’ kuzungumza,” alisikika mualikwa mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Hata hivyo, waalikwa wengi walipongeza kitendo hicho cha Idris kuwa bize na gauni la Madam kwani kilipendezesha shughuli hiyo ambapo mara kwa mara waalikwa walisikika wakiwashangilia wawili hao.

Paparazi wetu aliyekuwa akiwafotoa picha wawili hao tangu wakiwa jukwaani hadi waliposhuka, alifanikiwa kuzungumza na Idris na kumtaka atoe maoni yake kuhusu kuteswa na gauni hilo ambapo alisema ni suala la kawaida maana ilipangwa iwe hivyo.

“Yani hapa kila kitu kilipangwa kikapangika ndiyo maana unaona mimi nikawa namshikia gauni, namshika mkono na hata namna ya kutembea kama ulivyoona. Ni jambo la kawaida ambalo tulilipanga,” alisema Idris.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.