Video ya ‘Natafuta Kiki’ Yakwamishwa Na Wasanii Waliotajwa. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video ya ‘Natafuta Kiki’ Yakwamishwa Na Wasanii Waliotajwa.

Raymond
Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond aka RayVanny ameitaja sababu kubwa ya kuchelewa kwa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ kuwa ni baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo huo kushindwa kuonesha ushirikiano.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ wamekuwa wagumu kupatikana.
Aidha Raymond ameongeza kuwa menejimenti yake ilimleta director kutoka nje lakini baada ya baadhi ya wasanii kushindwa kuonesha ushirikiano wakamruhusu kurudi kwao kwanza.
Kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kuiona video ya wimbo huo, Raymond ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni Guitar Version. Hata hivyo Raymond amedai video hiyo itafanyika japo hajataja itachukuwa muda gani.


-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.