Stamina Kuja Na Remix ya “Mmeniroga” Ndani Yupo Roma & Jay Moe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Stamina Kuja Na Remix ya “Mmeniroga” Ndani Yupo Roma & Jay Moe

Kabwela mwenye kitambi ni nickname ya mwanahiphop mwenye asil ya Morogoro nayefanya vizuri kwa sasa na nyimbo yake ya “Mmeniroga” Stamina.

Staminah amethibitisha kuileta remix ya nyimbo hiyo ya Mmeniroga ambayo amefanya na wasanii wakali pia wa Hiphop Nchini Tanzania Roma na Jay Moe.

Akihojiwa na E News ya East Africa Television (EATV) Stamina amesema amewataka mashabiki zake wakae mkao wakula sababu muda wowote anawaletea Video na Audio vyote kwa pamoja vya Remix hiyo ya Mmeniroga.

Akiongea kwa msisitizo Stamina amesema kuwa anauhakika kuwa ngoma ni kali na ndio maana ameamua kuifanyia Video kali ili kuwapa burudani mashabiki zake.

Stamina anaiamini hiyo remix kias kwamba amethibitisha kuwa kuna uwezekano wa kuipoteza ile ya kwanza kwasababu watu aliofanya nao ni watu anaowaamini kwa 100%.

Video imefanywa na Msafiri wa Kwetu Studios. Kaa mkao wa kula kuisubiri Remix ya Mmeniroga kuroka kwa Stamina akiwashirikisha Roma na Jay Moe.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.