Snura: Chura Wangu Bado Ameshikiliwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura: Chura Wangu Bado Ameshikiliwa

MKALI wa wimbo wa Chura, Snura Mushi ‘Majanga’ amesema  bado wimbo wake umezuiliwa licha ya kupeleka muswada mpya unaoongoza video mpya ya wimbo huo.
Snura aliwaambia waandishi wa habari visiwani hapa wakati akijiandaa na show yake ya jana usiku katika tamasha la Ziff kwamba ameshapeleka marudio ya script ya pili aliyotakiwa afanye na mamlaka husika baada ya kwanza kukataliwa.
“Wimbo wangu wa Chura bado umezuiliwa lakini kwa sasa nina wimbo mwingine unaitwa ‘Shindwe’ ukimaanisha kishindo huu utaniongezea mashabiki kutokana na kuwa katika mahadhi ya uswahilini, kisingeli,’’ alisema
Aliongeza kwamba mashabiki wa ‘Chura’ waendelee kuvuta subira hadi mamlaka husika zitakaporuhusu video hiyo kurudiwa kwa kufuata maadili yanayotakiwa.
Onyesho la jana usiku lilikuwa maalum kwa kuitwa ‘Usiku wa Bi Kidude’ ambapo wasanii na majd walioshiriki katika burudani ni wanawake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.