Shaa Kutoa Video Mbili za Wimbo Wake Mpya ‘Sawa’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shaa Kutoa Video Mbili za Wimbo Wake Mpya ‘Sawa’

Mwanadada Shaa ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa sawa amesema anajipanga kuachia video mbili za wimbo huo kwa mara moja.

Akiongea kwenye mahojiano yake na kipindi cha daladala beats cha Magic Fm Shaa amesema video ya kwanza imefanywa na director Justin Campos wa Afrika Kusini na ya pili ambayo itakuwa ni dance video ya wimbo huo imefanywa na director Nick Dizzo.

“Video ya kwanza ni ya kirembo na Swaga zaidi,ambayo nimefanya na Justin Campos na hiyo ya pili ambayo nimefanya na director Nick Dizzo itakuwa ni dance video ili hata watu wakiwa club wajue wanachezaje” alifunguka Shaa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.