Roma Asema BASATA Haikuwahi Kuwa na Sababu za Msingi Kufungia Nyimbo Zake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Roma Asema BASATA Haikuwahi Kuwa na Sababu za Msingi Kufungia Nyimbo Zake.

Rapa anayefahamika kuwa na mashairi yenye utata anayeuwakilisha poa mkoa wa Tanga Ibrahim ‘Roma’ Mussa, amesema aliwauliza Baraza la sanaa Tanzania BASATA sababu ya kufungia nyimbo zake na mara zote amekuwa akipewa majibu yasiyoeleweka.

Roma amekiambia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm jana, Kuwa hawampi sababu za msingi zaidi ya kulitaja neno uchochezi ambao hawaufafanui kwa undani. “Sanaa yetu haina kanuni ndio maana unaona haya yanatokea, nilijaribu kuwauliza BASATA kwanini wameifungia wimbo wangu lakini sikupewa majibu ya msingi yenye kueleweka. “Najibiwa tu ‘Uchochezi’” Alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.