Roma Afafanua Mstari “Boss Amemganda Dangote,Ameisahau Tip Top” , Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Roma Afafanua Mstari “Boss Amemganda Dangote,Ameisahau Tip Top” , Ipo Hapa

“Boss amemganda Dangote,ameisahau Tip Top” kutoka kwa Roma ni moja kati ya mistari inayozungumziwa sana kwa sasa huku ikidaiwa kuwa Roma amemponda Babu Tale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Diamond na meneja wa Tip Top pia kwenye wimbo wake wa kaa tayari.

Kwa upande wake Roma amesema kuwa hakumaanisha kumponda meneja huyo kama watu wengi wanavyodhani bali alitaka kufikisha ujumbe kuwa watu wasisahau walipotoka lakini kwa njia ya kisanii zaidi.

“Tafsiri ya mstari huo ni kwamba tusisahau tulipotoka,ningeweza tu kuandika hivyo lakini kama msanii inabidi niwe mbunifu,ndio nikajenga hiyo picha na ndiyo maana watu wameukumbuka zaidi” alifafanua Roma alipokuwa akihojiwa na HZB TV.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.