Richard wa Big Brother Afunguka kuhusu Ukimya Wake, Yote Yapo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Richard wa Big Brother Afunguka kuhusu Ukimya Wake, Yote Yapo Hapa

Mshindi wa kwanza wa shindano la Big Brother Africa II mwaka 2007 Richard Bezuidenhout ametoa sababu za yeye kutoonekana kwenye tasnia ya burudani hapa Bongo.Mshindi huyo wa BBA ambaye pia aliwahi kutamba kwenye tasnia ya filamu nchini amesema ukimya wake ni kutokana na yeye kutokwepo nchini kwa muda mrefu.

Akiongea na Sam Missago kwenye kipindi cha FNL Richard amesema kuwa kwa sasa makazi yake yamehamia nchini canada ambapo pia anajihusisha na shughuli za uigizaji na tayari ameshafanya filamu yake akiwa nchini humo ambayo amekuja kuitangaza nchini Tanzania.

“Nilipotea kidogo kwa sababu nilihamishia makazi yangu Canada na huko pia nilikuwa najihusisha na filamu zaidi,sasa hivi nimekuja Tanzania kuitangaza muvi yangu nliyoifanya huko ambayo imechanganya watu wa nchi mabalimbali kama Kongo,Kenya,Rwanda na Burundi inayoitwa Mchumba sio ATM” alifunguka Richard ambaye aliweka wazi kuwa ukiachana na kazi zake za filamu binafsi ameshafanya usaili na kupata shavu la kuonekana kwenye moja ya Tv series za nchini humo ambao kwa sasa iko kwenye hatua za mwanzo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.