Madee Afunguka Haya Kuhusu Mstari wa Roma Kwenye Ngoma ya 'Kaa Tayari' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Madee Afunguka Haya Kuhusu Mstari wa Roma Kwenye Ngoma ya 'Kaa Tayari'

Rapper Roma Mkatoliki kupitia wimbo wake mpya ‘Kaa Tayari’ amekiibua kitu kilichopo lakini ambacho hakuna mhusika aliyewahi kukisema hadharani. Kitu hicho ni meneja wa Tip Top Connection, Babutale kuwekeza muda wake mwingi zaidi kwa Diamond na label ya WCB kuliko anavyofanya kwa kambi hiyo ya Manzese.
Kwenye wimbo huo, Roma anasikika akirap: “Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top.”
Muimbaji na mmoja wa wasanii wa miaka mingi wa Tip Top, Madee amesema wanautafakari mstari huo kama una ukweli na watakuja na jibu rasmi.
“Tumeusikia mstari wa @Roma_Mkatoliki na bado tunautafakari km unaukweli wowote…thn tutawajibu,” Madee ameandika kwenye Twitter.
Wiki iliyopita Said Fella aliuelezea mstari huo na kudai kuwa ni jambo ambalo amekuwa akimueleza Tale kuwa nalo makini.
“Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema, na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu. Lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK,” Fella
alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
Hadi sasa ni Madee na Dogo Janja pekee wamebaki kuwa wasanii wa Tip Top wanaosikika zaidi kuliko wengine. Kundi hilo limewahi kuwa na wasanii wakali wengine wakiwemo MB Dog, Tundaman, Cassim Mganga, Keisha, Z-Anto na wengine.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.