Kutazama TV kwa Muda Mrefu Kunasababisha Magonjwa Haya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kutazama TV kwa Muda Mrefu Kunasababisha Magonjwa Haya

Wanasayansi kutoka nchini Japan wamethibitisha kuwa kukaa kwa muda mrefu kwa kutazama TV kunasababisha ugonjwa ujulikanao kama ‘Fatal pulmonary embolism’.

Watafiti hao wameweza kugundua kuwa kukaa kwa muda mrefu kunasababisha kuganda kwa damu ambayo husukumwa kwa nguvu kwenye mzunguko wa damu na kwenda kuziba sehemu zilizokuwa wazi ndani ya mwili wa binadamu.

Wanasayansi hao walifanya uchunguzi huo kwa takribani miaka 19 kwa watu wasiopungua 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.

Matokeo hayo yalibaini kuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama TV ana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.