Kauli ya Nay wa Mitego Baada ya “Pale Kati Patamu” Kufungiwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kauli ya Nay wa Mitego Baada ya “Pale Kati Patamu” Kufungiwa

Ni siku chache tu zimepita baada ya hit maker wa nyimbo ya “Shika Adabu Yako” Nay wa Mitego kuachia nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la “Pale Kati Patamu”
Nyimbo ambayo imezua gumzo kubwa mtaani kwa kile kinachozungumzwa kuwa nyimbo hiyo haina maadili. Gumzo zilianza mapema baada ya picha za kava za nyimbo hiyo kutoka kabla nyimbo hiyo haijaachiwa rasmi ikiwa baadhi ya picha hizo ziliwaonyesha wadada wakiwa watupu (Hawaku vaa nguo).
Jumamosi ya July 16 Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko rasmi kuwa wameifungia nyimbo hiyo kwa sababu za ukosekanaji wa maadili katika nyimbo hiyo. Perfect255 imemvutia waya Nay wa Mitego (Imempigia simu) na kumuuliza juu ya swala hilo. Na haya ndio majibu ya Nay Wa Mitego.
“Nimeona hivyo vitu na ndio nataka nivifuatilie kwa sababu mimi sijatoa video ya huu wimbo na kava ya huu wimbo ni kava ambayo mimi nime ipost katika ukurasa wangu wa Instagram ambapo ndipo ninapatumia kwa ajili ya ku promote muziki wangu, vitu vingine tofauti havihusiani na mimi kabisa. Nina imani hawana matatizo tutakaa tutaelewana kwasababu nina imani ni watu waelewa, nitafuata utaratibu unao stahili nadhani nitajua nini cha kufanya baada ya hapo. Nahitaji wimbo wangu urudi na mashabiki zangu waendelee kuusikia.”
Nay Wa Mitego aliweka wazi kuhusiana na mipango aliyokuwa akiipanga kufuatana na wimbo huo kuwa ana mipango ya kushuti video nne kwa wimbo huo na hadi sasa tayari amekwisha kamilisha video mbili ambazo moja ameifanyia South Afrika na nyingine ameifanyia hapa hapa nyumbani.
“Wimbo wa Pale Kati utakuwa na video nne, na tayari nimesha shuti Video moja South Afrika na nyingine nimefanya hapa nyumbani, nimetumia gharama nyingi sana kufanya promotion ya Audio, hizi gharama zinapoteaje!? Mimi ni kijana ambaye nimejiajiri kupitia muziki” Alisema Nay wa Mitego.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.