Jokate Amfungukia Alikiba Asema Ni 'King wa Kweli' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jokate Amfungukia Alikiba Asema Ni 'King wa Kweli'

Msanii na mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kumwaga sifa za kutosha kwa msanii Alikiba na kusema kuwa ni msanii huyo ni mfalme ila hana mbwembwe kama wasanii wengine.
Jokate alitumia ukurasa wake wa Instagram kumwaga sifa hizo na kudai kuwa akiwa amenuna akisikia sauti ya Alikiba anajikuta anafurahi kwani anavutiwa sana na sauti hiyo.

“Alikiba ni King wa kutoa ngoma baada ya ngoma, King asiye kuwa na mbwembwe, ni mzuri kuliko wote, ni mfalme wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni. Nikinuna najikuta nafurahi nikisikia sauti yake, hapa nimesikiliza ‘Nisamehe’ nairudia tu, Nisamehe ni wimbo wa taifa unakuja kwa kasi ya ajabu”. Aliandika Jokate

Alikiba na Baraka the Prince wanategemea kuachia wimbo ambao utaiwa ‘Nisamehe’ ni wimbo wa Baraka the Prince ameshirikisha Alikiba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.