Joh Makini: Nachagua Sana Inapofikia Ishu ya Kufanya Kolabo, Vizego Ni Hivi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Joh Makini: Nachagua Sana Inapofikia Ishu ya Kufanya Kolabo, Vizego Ni Hivi.

Msanii wa hip hop kutoka kundi la Weusi Joh Makini amedai kuwa yeye huwa hafanyi kolabo tu na mtu yeyote bali huangalia mtu anayem feel.

Joh ameweka wazi kuwa umaarufu wa mtu kwake sio kigezo cha yeye kufanya naye kolabo bali huwa anaangalia mtu ambaye anayeendana naye ili waweze kutengeza muziki mzuri na kuongeza kuwa watu wengi wanamlalamikia kuwa anapotezea makolabo.

“Mimi niko very selective kwenye mambo ya kolabo..yani nachagua sana hata hapa bongo kuna malalamiko mpaka watu wengine wanakuuliza unataka shilingi ngapi,it’s not about the money,me naangalia mtu ambaye ninam feel,sio kwa sababu ana jina kubwa,nataka mtu ambaye tukiungana tunatoa muziki mzuri” alifunguka Joh Makini ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Perfect Combo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.