Gigy Money na Idris Sultan Sasa Mahaba Motomoto. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money na Idris Sultan Sasa Mahaba Motomoto.

Baada ya hivi karibuni penzi la Wema Sepetu na Idris kusambaratika, mwanadada Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kuchukua nafasi na sasa ni mapenzi motomoto.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Gigy Money na Idris kwa sasa ni mapenzi motomoto na mwanadada huyo aliamua kutafuta kazi ya utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM ili amnase Idris ambaye naye ni mtangazaji wa hapo.
“Idris na Gigy Money sasa ni mapenzi motomoto, alimfuata Choice (Choice FM) ili amnase vizuri na kweli amefanikiwa na hata kuachana kwa Idris na Wema kuna chembechembe za yeye kulivuruga penzi lao kwani baada ya kuachana ndiyo mapenzi yamekuwa motomoto sana,” kilisema chanzo.
Hivi karibuni Gigy Money alitundika picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na Idris huku akisindikizia na maneno kwamba ‘Hainaga ushemeji tunakulaga, leo niweke wazi kabisa jamani huyu ni mume wangu’.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Gigy Money ili kuupata ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Idris ameachana na Wema na nilijitahidi kutafuta kazi kwenye redio Choice ili niweze kumnasa vizuri na kweli nimefanikiwa, kiukweli nimejikuta nampenda sana. Sioni tatizo yeye ni mwanaume, mimi ni mwanamke, acha maisha yaendelee,” alisema Gigy.
Jitihada za kumpata Idris aweze kuzungumzia penzi hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
-gpl

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.