Enos Olik Atajwa Prodyuza Bora Kenya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Enos Olik Atajwa Prodyuza Bora Kenya

MTAYARISHAJI wa video za muziki nchini Kenya, Enos Olik, ametajwa kuwa ni bora katika kutayarisha video za wasanii mbalimbali ndani na nje ya Kenya.
Prodyuza huyo amefanya video za wasanii mbalimbali kama Nishike, Sura Yako, Still The One na Nerea za Sauti Sol, Kioo (Jaguar), Ivo Ivo (Octopizzo), Come Over (Vanessa Mdee), Pamoja (P-Unit) na wasanii wengine wengi.
Katika watayarishaji watano bora nchini Kenya,  kati ya Young Wallace, J Blessing, Thomas Mboss, Sammy Dee, Olik ametajwa kuwa ni bora zaidi katika video za kisasa.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Olik, gharama zake zimekuwa juu tofauti na wengine kutokana na ubora wa kazi zake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.