Dancer wa Koffi Olomide Akanusha Kupigwa Kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyata - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dancer wa Koffi Olomide Akanusha Kupigwa Kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyata

Baada ya mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide kukamatwa jana kwa kumpiga teke dancer wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi, Dancer wake huyo aliyepigwa anayejulikana kwa jina la Pamela amekanusha kuwa Koffi Olomide hakumpiga.
Koffi alikuwa anatarajiwa kutumbuiza leo katika uwanja wa Bomas, ndipo tukio zima la kumpiga dancer wake likatokea baada ya kumkosea heshima mpenzi wake Cindy Le Couer ambaye ni muimbaji wa bendi yake.
Lakini taarifa zingine za upande wa pili wa dancer wake huyo anayejulikana kama Pamela, alitumia kurasa yake ya facebook kukanusha juu ya tukio hilo kuwa hitmaker wa ngoma ya Selfie, Koffi Olomide hakumpiga, wakati tukio zima lilikuwa limenyakwa na kamera.
“Dear fans of Koffi Olomide, I would like to tell you that Koffi did not attack me, it was a girl at the airport that was threatening me and Koffi came to defend me…Koffi can never beat us in public, and we all know that Koffi loves his dancers and he can never do something like that,” alisema Pamela kupitia video iliyopostiwa facebook.
Dancer huyo aliongeza kuwa Koffi huwa anakawaida ya kuwapiga na mtu ambaye sio mkorofi.
“For your information, Koffi does not beat us. For all those who love Koffi, I want to tell you that Koffi is not someone who is aggressive… he loves us very much and it’s just a girl who came and started attacking us. As far as we are concerned, we don’t have any problem. We came for a concert. We are in good terms with Koffi. He is our president and he never harms us.”alisema Pamela Dancer wa Koffi.
Koffi Olomide alikamatwa nje ya studio za Citizen TV baada ya video ya tukio la kumpiga dancer wake wa kike kusambaa katika mitandao ya kijamii, hivyo inspector Joseph Boinnet kuagiza askari polisi wamkamate mwanamuziki huyo mkongwe. taarifa zinaeleza Koffi amekamatwa na kupelekwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudishwa kwao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.