Chidi Benz: Mr Blue Alillia Machozi Kila Alipokuwa Akiniona Nateseka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chidi Benz: Mr Blue Alillia Machozi Kila Alipokuwa Akiniona Nateseka

Kwa mujibu wa Chidi Benz, watu wote walikuwa na uwezo wa kumwacha na kumchoka katika majaribu aliyoyapitia, lakini si Mr Blue
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM wiki iliyopita, Chidi alisema kuwa Blue ni rapper aliyemsaidia bila kuchoka na anamchukulia kama mdogo wake special.

Amedai kuwa mara nyingi alikuwa akikutana naye na kuanza kulia kwa jinsi alivyokuwa amedhoofika. “Ila tukikutana naye sasa anaweza akaongea mara akaanza kulia hicho ndicho alikuwa ananiboa,” alisema rapper huyo.

Amedai kuwa Blue alikuwa akitumia muda mwingi kumpa ushauri bila kuchoka.

“Hata kesho he is there for me, he is my young brother, I respect him, I salute him, I am there for him too, whatever he needs I provide,” alisisitiza rapper huyo.

Kwa upande wa Diamond, Chidi amedai kuwa naye amemfanyia mambo mengi makubwa ikiwemo kumlipia takriban milioni 27 kwaajili ya gharama za hospitali kumsaidia aachane na madawa ya kulevya.

“He did it like two times, three times, mpaka akafikia time akawa anakasirika sasa ndio maana this time he is happy, nipo hapo WCB narekodi nyimbo, he is happy.”

Chidi ameachia wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliomshirikisha msanii wa WCB, Raymond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.