Bill Nas "Sijawahi Kumtamani Shilole, Namwona Kama Mshkaji Wangu wa Kiume" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bill Nas "Sijawahi Kumtamani Shilole, Namwona Kama Mshkaji Wangu wa Kiume"

Rapper Bill Nas ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Chafu Pozi amekanusha tetesi za kuwa anatoka kimapenzi na staa wa kike wa Bongo Fleva na filamu,Shilole.

Akijibu swali hilo kwenye moja ya mahojiano yake rapper huyo amedai kuwa hajawai kumtamani Shilole licha ya kuwa huwa wanashinda wote siku nzima kitu kinachotafsiriwa vingine na watu na kuongeza kuwa yeye anamwona kama mshikaji wake wa kiume

“Shilole ni mshikaji wangu wa siku nyingi hakuna chochote kinachoendelea,tuna hang out sana.Nikiwa nae najisikia kama niko na mchizi wangu kama mwanaume mwenzangu yaani kama dada yangu,sijawahi kumtamani wala sijawahi kumfikria hivyo..naweza kushinda naye siku nzima hata mpaka saa nane za usiku,nampeleka studio..” alifunguka rapper huyo na kudai kwa sasa hayuko kwenye mahusiano na mtu yeyote.

-Magic Fm

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.