Avril Afunguka Kuhusu Skendo ya Kugawa Uroda Kwa Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Avril Afunguka Kuhusu Skendo ya Kugawa Uroda Kwa Diamond

Avril mwanamuziki kutoka Kenya ametua Bongo kimya kimya ambapo zile skendo za kuwa huenda Diamond Platnumz baada ya video ya ‘Kesho’ waliyoifanya miaka ya nyuma labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye kimapenzi.

Avril kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alisema kuwa yeye na Diamond Platnumz hawakufanya project nyingine yoyote zaidi ya kutengeneza video ile ya ‘Kesho’ japo alimuelezea Diamond kuwa ni msanii mpole sana na mwenye kupenda kazi yake na kujituma.

“Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu. Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya” alisema Avril

Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.