Augustino Mrema Alamba Kutoka Kwa Rais Magufuli. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Augustino Mrema Alamba Kutoka Kwa Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempa shavu mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema kwa kumteua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai 16.

Mrema akiwa na Rais Magufuli wakati wa kampenzi za uchaguzi uliyopita

Mrema ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani wakati awamu ya pili, amekuwa akimwomba Rais Magufuli ampe kazi aliyomwahidi alipojitokeza kwenye kampeni zake na kumpigia debe.

Mbali na Mrema anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Eusebia Munuo ambaye muda wake umemalizika, Dk Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi nyingine mbalimbali na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Wengine walioteuliwa ni Profesa William R. Mahalu ana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.