Wolper na Nisha wazinguana kisa Harmonize? Nisha kajiweka kwa Raymond? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wolper na Nisha wazinguana kisa Harmonize? Nisha kajiweka kwa Raymond?

Wolper
Drama za mastaa wa bongo movies hazeshi (no typo). Jacqueline Wolper na Salma Jabu maarufu kama Nisha wamepishana lugha huku Harmonize akiwa chanzo.
Wolper
Issue ilianza vingine kabisa. Nisha alipost picha inayowaonesha Ben Pol, Raymond, Nuh Mziwanda na Rich Mavoko na kuandika: Mmoja kati ya hawa amejaa kwenye galary ya simu yangu na moyoni mwangu,otea A B C AU D? enhe. he sa hv siweki hadharani maana nna phd ya kunyakuliwa, sa hivi ni kumpost kwa mwendo kasiii yaani wengi wengi simtaji ng’ooo.
Watu walicheka, walifurahi na kucomment hadi pale comment ya mwana bongo movie mwenzake, Jacqueline Wolper ilipobadilisha kabisa hali ya hewa.
13413370_190305564700163_1704982609_n
13413370_190305564700163_1704982609_n
Nisha alilazimika kuitolea ufafanuzi comment ya Wolper na ndipo mambo yaliyopo nyuma ya pazia yakawekwa hadharani. Seems like Nisha aliandaa show Mtwara na kumchukua Harmonize hali iliyomfanya Wolper naye aende Mtwara – of course kulinda chake kisijekupokonywa!
“Ok guys kuna picture niliweka saa 4 asbh leo,za wasanii kadhaa wa music ambao niliweka na caption yangu kwa furaha zangu tu,” aliandika Nisha kwenye post nyingine.
“Ila baada ya lisaa limoja ikaja coment hiyo ya msanii mwenzangu sikudhungumza chchte,i was like ok nikacheka tu. Then zikaja comments nyingi za kumuuliza kulikoni kuandika hivyo. Masaa mawili yaliyopita ukaandikwa waraka mzito mrefu unaosema. “Nisha aandaa show Mtwara ya kumnasa Harmonize ila Wolper akagundua hilo akaamua kuongozana naye Harmo hadi huko kukwepa hilo (NA MANENO MENGI YA ZIADA YA UONGO.”
“Ikimbukwe show imeshapita km week na haya maneno yamezuka leo baada ya hiyo comment. Guyz tuje kwenye point KWANZA KABISA SIJAMLENGA YYTE KWA NILIYEANDIKA NILIANDIKA KWA MAPENZI YNG KM NILIVYOANDIKA JANA STATUS YA VIDONDA VYA TUMBO,TENA HADI WADOGO ZNG NIKAWAAMBIA TAZAMA NACHEZA NA AKILI ZA WATU. NIMESHANGAA HABARI ZA UONGO KUSAMBAZWA ZIDI YANGU TENA BAADA YA COMENT HII KWANGU,” aliongeza.
“POINT YA PILI KWA YYTE ANAYEULIZA NIMEANZA LINI UPROMOTA guyz mimi ni mfanyabiashara na kwenye pesa nipo,show ya MTWARA imenigharimu si chini ya ml.18 unadhani naweza poteza pesa zote hizo kisa mapenzi?sina ujinga huo wa akili. NA SIJAWAHI KUMTAKA NA SITOTARAJI KWANZA SIJAZOEA KUPITA ANAPOPITA MTU HASWA NNAYEMJUA.”
“TATU nimeandaa show ingine ramadhan ya 13 DAR-ES-SALAAM inahusu ramadhan, nna SHOW SKUKUU YA IDD MOSS NA IDD PILI MIKOANI ZOTE MM NDO MUANDAAJI NA KUNA WASANII WAKUBWA TU JE HAO PIA NATAKA KUWANASA? HE. IFIKE HATUA TUSIWE TUNABALANCE MTU MMOJA NA PIA SIO KILA ASIYEDHUNGUMZA NI MNYONGE SANA ILA KUNA WKT DRAMA HAZINA MUDA INABIDI UPIGE KAZI MAANA MAISHA YANAENDA MBELE HAYARUDI NYUMA. NB:SHUKRAN KWA WEWE UNAYESAMBAZA UJUMBE HUU WA UONGO SINA CHA KUKWAMBIA NIMEPITIA MENGI MAKUBWA SO HILI KM NACHEZA MDAKO. (mwenye uelewa kaelewa chanzo cha story inayosambaa imetoka wapi,nimeandika hapa kwa manufaa ya mashabiki zangu wote watakaobahatika kusoma habari hizo za uongo.”
Na sasa hebu turejee kwenye post ya mwanzo kabisa ya Nisha. Ni msanii gani kati yao hao wanne ambaye yupo moyo mwake kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe? Tuanze kudadafua:
BEN POL
Hapana, juzi tu ametoka kuwa baba na mwanae anaitwa Mali aliyezaa na mchumba wake wa muda sasa Latifa Mohamed. Jamaa ni mwaminifu.
NUH MZIWANDA
Hapana, juzi tu ameanza kumuonesha mpenzi wake ambaye tayari amejichora tattoo yake. Sio rahisi!
RICH MAVOKO
Hapana, juzi tu mwanae amefikisha siku 40 na kumtoa nje kwa mara ya kwanza na Diamond alikuwepo. Ni ngumu.
RAYMOND
Ewalaaah.. tunaweza kumfikiria hitmaker huyu wa Kwetu kwasababu hadi sasa hajamweka hadharani mpenzi wake.
Ifahamika tu kama alivyosema Nay wa Mitego.

Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.