Wazazi wa Madee Wamkomalia Avute Jiko, Majibu Yake ni Haya ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wazazi wa Madee Wamkomalia Avute Jiko, Majibu Yake ni Haya !

STAA wa Wimbo wa Migulu Pande, Hamad Ally ‘Madee’ amesema hakuna kitu kinachomtesa kwa sasa kama ombi la wazazi wake wanaomtaka avute jiko huku wakidai umri wake unazidi kusonga mbele jambo ambalo anatakiwa kulitazama kwa jicho la tatu.

Akichonga kiaina na gazeti hili, msanii huyo mwenye mtoto wa miaka 8 aitwaye Saida alisema, siku za hivi karibuni suala hilo limekuwa kama wimbo wa taifa kwa wazazi wake lakini jibu analowapa ni kuwa muda wake muafaka haujafika na ukifika ataoa tu.

“Watu huwa wanashindwa kuelewa kuwa suala la kuoa huja automatical, hakuna atakayenilazimisha kufanya hivyo ingawa suala hilo linanitesa sana maana ninatamani kuwaridhisha wazazi wangu,” alisema Madee.

Alipoulizwa juu ya sababu hasa zinazosababisha asivute jiko, Madee alisisitiza kuwa muda wake wa kuoa haujafika na kwamba kwa sasa yupo bize na mambo yake mengine.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.