Tiwa Savage: Roc Nation ni Zaidi ya Muziki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Tiwa Savage: Roc Nation ni Zaidi ya Muziki

NYOTA wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, amesema maisha anayoishi katika lebo yake mpya ya Roc Nation ilio chini ya rapa Jay Z ni zaidi ya muziki.

Wiki iliyopita msanii huyo alipata dili ya kusaini mkataba na kampuni ya Roc Nation, ambapo atakuwa anasimamiwa kazi zake zote za muziki chini ya Jay Z.

Aprili 2015, Jay Z alisema kwamba anatarajia kutafuta vipaji nchini Nigeria na sasa Tiwa amekuwa msanii wa kwanza nchini humo kusaini mkataba huo.

“Ni kama ndoto kusaini mkataba na kampuni kubwa kama Roc Nation ambayo ina msanii mwenye uwezo mkubwa, lakini furaha nyingine ni kwamba ninafurahia maisha ya Roc Nation kwa kuwa ni zaidi ya muziki, kuna mambo ninajifunza na nakutana na watu mbalimbali ambao sikuwatarajia,” alisema Tiwa.

Roc Nation ilianzishwa mwaka 2008, huku kukiwa na idara mbalimbali kama vile maprodyuza, waandaaji wa vipindi vya runinga, wasanii na mambo mengine mengi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.