Snura: Wimbo wa Chura Ndio Unaowanyamazisha Watu Jukwaani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura: Wimbo wa Chura Ndio Unaowanyamazisha Watu Jukwaani.


Na Abdallah Mchande
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi amesema licha ya nyimbo yake ya chura kufungiwa na Wizara ya habari, sanaa na michezo kwa kuonekana hauna maadili lakini wimbo huo ndio huwanyamazisha watu unapopigwa kwenye show.
Snura ameyasema hayo kwa mashabiki zake wakati akifanya show iliyofanyika katika klabu ya Entebe mjini Zanzibar.
"Huu wimbo (chura) wanasema hauna maadili lakini ndio huwanyamazisha watu unapopigwa kwenye show"
.
Snura aliu-perform wimbo huo wa chura katika show yake hiyo kwa kucheza mdundo wa nyimbo tu pasipo kuimba mashairi yake, ikiwa ni hatua ya kutii zuio lililotolewa na Wizara kumzuia Snura kuutumia wimbo huo katika show zake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.