Sirro: Tunamuhitaji Askofu Gwajima - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sirro: Tunamuhitaji Askofu Gwajima

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo linamuhitaji Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa kuwa kuna mkanda wameupata unaosemekana ni wake ambao unazungumza maneno ya kichochezi.

Kamanda Sirro alisema: “Tumepata clip (mkanda) inayosemekama ni ya kwake. Tunamtaka athibitishe kama hayo maneno ni ya kwake. Na kama ni yeye ameyasema, anaelewa nini kuhusu kile alichokizungumza kwa sababu hayo maneno ni kichochezi. Tupo kwenye uchunguzi mama yangu.”

Jana, polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.

chanzo: mwananchi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.