Shetta: Gharama ya Video ya Wimbo ‘Namjua’ ni Sawa na Pesa ya Kununua Nyumba 2 Mbagala. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shetta: Gharama ya Video ya Wimbo ‘Namjua’ ni Sawa na Pesa ya Kununua Nyumba 2 Mbagala.

Msanii wa muziki, Nurdin Bilali ‘Shetta’ amefunguka kwa kusema kuwa gharama aliyotumia kuandaa video yake mpya ya wimbo ‘Namjua’ angeweza kununua nyumba mbili Mbagala jijini Dar es salaam.
Akiongea na wadau mbalimbali waliyojitokeza katika uzinduzi wa management yake mpya Alhamisi hii ndani ya Hyatt Regency Hotel, Shetta amesema video ya wimbo ‘Namjua’ imemcost pesa nyingi kuliko video zake ambazo amewahi kuzifanya.

“Muziki sasa hivi umebadilika sana, tunawekeza pesa nyingi sana kwenye kazi, video ya wimbo ‘Namjua’ imegharimu pesa nyingi sana mpaka ukifikiria unaweza ukaumwa kichwa, yani gharama yake unaweza hata nunua nyumba mbili Mbagala na maisha yakaendelea. Lakini haya yote tunafanya kwa ajili ya kuusukuma mbele muziki wetu,” alisema Shetta.

Shetta alisema hataki tena kurudi nyuma katika muziki wake kwani atahakikisha anaendelea kufanya kazi nzuri ambazo zitaweza kuusogeza muziki wake mbele,

Pia Shetta aliitambulisha management yake mpya inayoongonzwa na Michael Mligwa aka MxCarter.

Shetta kwa sasa anafanya poa na video yake ya wimbo ‘Namjua’ ambayo alishoot Afrika Kusini.

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.